Kijarida Cha Kuelimisha Jamii Juu ya Masuala ya Ardhi

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi iko katika mchakato wa kupitia na kurekebisha Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995. Mpaka kufikia mwezi Novemba 2016 Wizara ilikuwa imetoa rasimu ya muswada wa marekebisho ya Sera ya Ardhi ya 1995. Aidha, Wizara kupitia timu ya wataalamu, iliendelea kukusanya na kupokea maoni na ushauri toka kwa wadau mbalimbali juu ya maudhui na mapendekezo ya marekebisho katika sera. Ikiwa rasimu hii ya sera itapitishwa, ni dhahiri kuwa kutahitajika pia marekebisho ya sheria za ardhi na sheria za kisekta zinazohusiana na matumizi, usimamizi, utawala wa rasilimali ardhi na utatuzi wa migogoro ya ardhi. Download

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *