Skip to main content
x
LARRI

TAARIFA KWA UMMA: MRADI WA KUSAIDIA KATIKA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI NA KUPATA VYETI VYA HAKIMILIKI YA KIMILA KATIKA VIJIJI 9 KATIKA MIKOA YA ARUSHA, MANYARA NA IRINGA.

Taasisi ya HAKIARDHI ni Asasi ya Kiraia iliyoanzishwa mwaka 1994 chini ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2002 kwa usajili namba 00NGO/R2/00012 wa mwaka 2019.  

HAKIARDHI ilianzishwa kwa lengo la kufanya Utafiti na Utetezi wa haki za ardhi kwa wazalishaji wadogo nchini ili kukuza uelewa wao katika kutetea haki za ardhi ambazo ni kupata, kutumia na kumiliki ardhi. Vilevile, Taasisi hushirikisha jamii za Wazalishaji wadogo taarifa mbalimbali za masuala ya ardhi na mabadiliko ya tabia nchi ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi na ya wakati kuhusu shughuli zao za uzalishaji zinazotegemea ardhi. 

Mnamo Januari 30, 2025 HAKIARDHI ilisaini mkataba wa ufadhili na Shirika la Trias Tanzania kwa lengo la kutekeleza mradi unaofahamika kwa jina la " Kusaidia katika Mpango wa Matumizi ya Ardhi na kupata Vyeti vya Hakimiliki ya Kimila katika vijiji 9 katika mikoa ya Arusha, Manyara na Iringa. ".  

Bajeti ya mradi huu ni Euro 35,000.00 ambazo ni sawa na Tsh89,955,250/= na utatekelezwa kati ya mwezi 01 Februari 2025 hadi 31 Julai 2025.

Imetolewa na uongozi wa Taasisi.