Taasisi ya Utafiti na Utetezi wa Haki za Ardhi (LARRRI/HAKIARDHI) ni Taasisi ya Kiraia iliyoanzishwa mwaka 1994 kwa lengo la kufanya Utafiti na Utetezi wa haki za ardhi kwa Wazalishaji Wadogo wadogo nchini ili kukuza uelewa wao katika Sera na Sheria za ardhi na kuimarisha mifumo ya usimamizi, matumizi na utatuzi wa migogoro ya ardhi. HAKIARDHI ilisajiliwa chini ya Sheria ya Makampuni Sura ya 212 mwaka 1994 na kisha mwaka 2019 usajili ulihamishwa chini ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali kwa usajili namba 00NGO/R2/00012.
HAKIARDHI is inviting interested Journalists to produce articles on land rights and climate change.
Mtandao wa Mashirika yanayojihusisha na Utetezi wa Rasilimali Ardhi (TALA) pamoja na wadau wengine walikutana Jijini Dar es Salaam kufanya uchambuzi wa Rasimu ya Mapitio ya Sera ya Taifa ya Ardhi 2016.