Tasisi ya HakiArdhi inakukaribisha kutembelea maktaba iliyoboreshwa yenye machapisho mbalimbali
SIKU: JUMATATU - IJUMAA
MUDA: 3:00 ASUBUHI - 11:00 JIONI
MAWASILIANO: 0784646752
Heri ya siku ya Muungano, 26 Aprilli 2021.
Miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzinbar.
"Muungano wetu ni msingi imara wa mapinduzi ya kiuchumi, tudumishe mshikamano wetu."
Taasisi ya Utafiti na Utetezi wa Haki za Ardhi (LARRRI/HAKIARDHI) ni asasi ya Kiraia iliyoanzishwa mwaka 1994 na mwaka 2019 ikasajiliwa kwa usajili namba 00NGO/R2/00012 chini ya Sheria ya Asasi za Kiraia ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.
Lengo la kuanzishwa kwa HAKIARDHI ni kufanya utafiti na utetezi wa haki za ardhi kwa wazalishaji wadogo nchini ili kukuza uelewa wao katika utekelezaji wa Sera na Sheria za ardhi ili kuimarisha mifumo ya usimamizi, upatikanaji, mipango ya matumizi na utatuzi wa migogoro ya ardhi.
Bodi ya Wakurugenzi, Wanachama, Menejimenti na Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti na Utetezi wa Haki za Ardhi (HAKIARDHI) tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya majonzi ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi 2021.
The Land Rights Research and Resources Institute (LARRRI/HAKIARDHI) is a non-governmental not for profit organization that was established in 1994 in recognition of the need to facilitate the realization of a socially just and equitable national land tenure system that promotes and advances the rights to the land of majority rural-based small producers such as peasants, pastoralists, artisan miners and other related groups.
Historia ya siku ya Wanawake duniani inaonesha kuwa tarehe 8 Machi ilichaguliwa kusherehekea siku ambayo wanawake katika Urusi ya Usoviet walianza kufanya maandamano ya haki ya kupiga kura ambayo walipewa mnamo 1917. Kwa hiyo ni sahihi kusema kuwa chimbuko la siku ya wanawake iliadhimishwa tu na wanaharakati wa kijamaa na nchi za kikomunisti. Ilipofika miaka ya 1960 hususani mwaka 1967 vuguvugu kubwa la wanawake (Feminist movement) walianza kuitumia siku hii kuadhimisha siku ya wanawake.
Taasisi ya HAKIARDHI imefanya uchambuzi wa bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya mwaka 2020/21 ili kubaini ni kwa kiasi gani bajeti hiyo inakidhi mahitaji ya wazalishaji wadogo hususani wanawake katika upatikanaji wa ardhi, matumizi, umiliki na utatuzi wa migogoro ya ardhi.